Show simple item record

dc.contributor.authorMutwiri, Fred John
dc.contributor.authorDkt. Musyimi, Dorcas
dc.date.accessioned2025-02-27T07:03:44Z
dc.date.available2025-02-27T07:03:44Z
dc.date.issued2023-02-02
dc.identifier.issn2663-3183
dc.identifier.urihttp://repository.lukenyauniversity.ac.ke/xmlui/handle/1/96
dc.description.abstractFasihi ya Kiswahili ya watoto kama taaluma haina muda mrefu katika historia ya fasihi ya Kiswahili. Ikilinganishwa na fasihi ya watu wazima ambayo ilianza muda mrefu, na pia tafiti nyingi kufanyika katika mataifa mengi. Fasihi ya watoto inaonekana kuwa imetelekezwa kwa muda mrefu kutokana na kutokupewa umuhimu unaostahili na wahakiki na hivyo kudharauliwa na wanajamii (Bakize, 2013). Wanajamii wengi wamekuwa wakiinasibisha fasihi hii na mambo ya kitoto ambayo ni rahisi, yasiyo ya msingi sana; na ndiyo maana inaitwa fasihi ya watoto (Wamitila, 2008). Tafiti zinaonyesha kwamba fasihi hii imechipuka barani Afrika hivi karibuni, hasa kwenye miaka ya 1980 kutokana na sababu kadhaa lakini mojawapo ikiwa ni kutiliwa mkazo kwa masuala ya haki za watoto (Ngugi, 2016a). Mulokozi katika Semzaba (2008) anaeleza kwamba nchini Tanzania, fasihi ya watoto ilichipuka wakati na baada ya ukoloni katika miaka ya 1960 na kushika mizizi miaka ya 1970. Zaidi ya hayo, fasihi hii ilishika mizizi zaidi miaka ya 1990 baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa Vitabu vya Watoto Tanzania. Nchini Kenya, fasihi ya watoto imepata umaarufu miaka ya 2000 baada ya kujumuishwa katika somo la Kiswahili kuanzia shule ya msingi hadi sekondari. Vilevile, hatua ya serikali ya kugharimia masomo imechangia sana katika maendeleo haya kwa sababu serikali ilichukua jukumu la kununua vitabu vya ziada na kiada. Makala haya yanalenga kutathmini ndumi za fasihi ya watoto kwa kurejelea maendeleo ya fasihi ya Kiswahili ya watoto kwa kufanya ulinganishi katika nchi za Tanzania na Kenya. Nchi hizi zimeteuliwa kwa sababu, kwa mujibu wa utafiti wa awali, fasihi ya Kiswahili ikiwa ni pamoja na fasihi ya watoto ya Kiswahili imepamba moto zaidi katika nchi hizi mbili za Afrika Mashariki kuliko nchi nyingineen_US
dc.description.sponsorshipLukenya Universityen_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherLukenya Universityen_US
dc.subject: Dhamira, Nduni, Watoto, Uhalisia.en_US
dc.titleNDUNI ZA FASIHI YA WATOTO KATIKA UWASILISHAJI WA DHAMIRA: KIELELEZO CHA SUNGURA MPANDA NGAZI NA SITAKI IWE SIRI.en_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record