dc.description.abstract | Haki za watoto ni suala ambalo limepewa uzito katika jamii mbalimbali ulimwenguni. Umoja wa kimataifa katika mwaka wa 1948, ibara ya 25 ulitambua utunzaji maalum wa mama na mtoto katika jamii. Watoto walipewa nafasi ya kuhutubia umoja huo kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 2002 kwenye makao makuu ya umoja huu mjini Newyork. Kutokana na shinikizo za kimataifa na mashirika mbalimbali yanayotetea haki za watoto, serikali za ulimwengu zimeweka vipengele maalum za kikatiba za kulinda watoto. Nchini Kenya sheria maalum kuhusu haki za watoto ilipitishwa katika mwaka wa 2001. Sheria hii inamfafanua mtoto kama binadamu yeyote aliye chini ya umri wa miaka kumi na minane. Aidha sharia hii inatetea haki za watoto na kupiga marufuku unyanyasaji wowote dhidi yao. Inatoa haki kama vile elimu, afya, malezi bora, haki dhidi ya ajira ya watoto, haki ya kulindwa wakati wa vita, haki ya kulindwa dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya, haki ya kucheza na kupewa nafasi ya kupumzika, utunzaji wa watoto wenye ulemavu miongoni mwa mengine. Sheria hii imeendelea kuimarishwa na kuhusisha vipengele vingine muhimu hasa baada ya katiba mpya ya mwaka
wa 2010 nchini Kenya. Haki za watoto ni suala ibuka lililopewa kipaumbele na wanajamii wote. Hatuwezi kuzungumzia haki za binadamu bila kugusia haki za watoto. Kutokana na mkabala huu, wanafasihi wengi pia wamejihusisha na maandishi mbalimbali yanayohusu haki za watoto. Makala hii inalenga kuchunguza jinsi riwaya za S. A. Mohammed zinavyoangazia haki za watoto na kuwalinda dhidi ya unyanyapaa. Mtaalamu huyu ni miongoni mwa wanariwaya wa visiwani ambao wameendelea kuacha taathira kubwa katika utanzu wa riwaya ya Kiswahili. Said A. Mohamed ameandika riwaya nyingi katika vipindi tofauti. Kazi nyingi za Mohammed zimekuwa na maudhui mengi yaliyohusu unyanyasaji na utetezi wa haki za watoto kutokana na utafiti wetu wa awali. Riwaya zake zilizochapishwa kufikia uandishi wa makala hii ni: Asali Chungu (1977), Utengano (1980), Dunia Mti Mkavu (1980), Kiza Katika Nuru (1988), Tata za Asumini (1990), Babu Alipofufuka (2001), Dunia Yao
(2004), Nyuso za Mwanamke (2010), Mhanga
Nafsi Yangu (2012), Mkamandume (2013), Kamwe si Mbali Tena (2014) na Wenye Meno (2018). Utunzi wa S. A. Mohammed unaweza kuangaliwa katika awamu mbili. Awamu ya
kwanza ni kazi zake zilizojifunga kwenye masuala ya jamii yake ambapo aliihakiki na kubainisha migogoro iliyotokota ndani. Kazi hizi zimejifunga katika ufafanuzi wa hali kama inavyobainika katika ulimwengu halisi na masuala ambayo yanaweza kudhihirika kihistoria. Riwaya zake za awamu ya kwanza ni pamoja na Asali Chungu, Utengano, Dunia Mti Mkavu, Kiza Katika Nuru na Tata za Asumini. Katika awamu ya pili anaandikia masuala ambayo yanahusu ulimwengu halisi na ulimwengu wa kiajabu ambapo mpaka wake hauwekwi bayana. Baadhi ya kazi hizi ni pamoja na Babu alipofufuka, Mkamadume, Kamwe si mbali tena na wenye meno Makala hii itajifunga katika kazi za awamu ya kwanza kwa kurejelea riwaya zake tatu mathalan: Asali Chungu, Kiza Katika Nuru na Tata za Asumini. Riwaya hizi ziliandikwa katika miongo mitatu tofauti na zinaweza kutupa taswira kamili kuhusu haki za watoto na namna jamii imekuwa ikizishughulikia katika vipindi mbalimbali vya kihistoria. | en_US |