• Login
    View Item 
    •   DSpace Home
    • Undergraduate Projects and Publications
    • LUKENYA UNIVERSITY MULTI-DISCIPLINARY JOURNAL
    • View Item
    •   DSpace Home
    • Undergraduate Projects and Publications
    • LUKENYA UNIVERSITY MULTI-DISCIPLINARY JOURNAL
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    UBABEDUME KATIKA TAMTHILIA YA BEMBEA YA MAISHA (2022)

    Thumbnail
    View/Open
    dorcas m article.pdf (312.6Kb)
    Date
    2023-02-02
    Author
    Musyimi, Dorcas M.
    Nyagah, Shadrack K
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Mfumo-dume humpa thamani kubwa mwanamume huku ukimdhalilisha mwanamke kwa sababu ya jinsia yake. Imani hii dunishi imo katika itikadi na tamaduni zinazohimiliwa na mfumo wa muundo wa kijamii ambao mwanamume anapewa nguvu na uwezo zaidi dhidi ya mwanamke katika nyanja zote za maisha hususan kiutawala, kiuchumi, kidini, kisiasa na kijamii. Basi, makala hii ililenga kuchunguza jinsi mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha (2022) alivyomsawiri mhusika wa jinsia ya kiume katika kazi yake ili kuweka wazi shughuli za ubabedume zilizojengwa katika mila, itikadi na utamaduni wa jamii husika. Data ya makala ilipatikana kwa kuisoma tamthilia teule kisha kuichanganua kwa kutumia Nadharia ya Ubabedume ambayo hulenga kubainisha nguvu na mamlaka yanayomilikiwa na jinsia ya kiume, hasa kutokana na utamaduni wa jamii husika. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa mhusika wa jinsia ya kiume amesawiriwa kama mtegemezi, mrithi wa mali, ameruhusiwa kupata mtoto nje ya ndoa, haruhusiwi kujishughulisha na kazi za nyumbani, anaitwa gumba kwa kutopata watoto na anayejitwika majukumu yote ya nyumbani. Masuala haya yamekithiri katika jamii za leo. Ikiwa nchi zinazoendelea zitapiga hatua katika maendeleo, basi usawa wa kijinsia unahitaji kutiliwa maanani na jamii zote.
    URI
    http://repository.lukenyauniversity.ac.ke/xmlui/handle/1/90
    Collections
    • LUKENYA UNIVERSITY MULTI-DISCIPLINARY JOURNAL [46]

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV
     

     

    Browse

    All of DSpaceCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV